Subscribe Us

MBUNGE NDEGE AKABIDHI VITI MWENDO KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Ndege, akiwa amembeba mtoto wakati wa hafla ya kutoa msaada wa viti mwendo kwa watoto wenye mahitaji maalumu Januari 11, 2026.

.......................................

Na Mwandishi Wetu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Ndege, Januari 11, 2026 amekabidhi viti Mwendo kumi  kwa watoto wenye mahitaji maalum kutoka kata mbalimbali za Babati Vijijini, kwa lengo la kuwasaidia kwa matumizi hasa wakati wa kwenda shuleni.

Hatua ya kutoa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihimiza kuisaidia jamii hasa waliopo kwenye kundi maalumu wakiwepo watoto wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo Mhe. Ndege alisema viti hivyo vitawawezesha watoto hao kwenda shule na wakiwa majumbani kwao.

Aidha, Mhe. Ndege ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha viti hivyo havifanyiwi biashara, bali vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa. 

Amewaomba wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu majumbani, akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha mazingira ya elimu kwa kuandaa shule zinazojumuisha watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo ulemavu wa viungo na ulemavu wa akili, hivyo watoto hao wapelekwe shule wasome kwani wana haki ya kupata mahitaji yote ya kibinadamu ikiwemo elimu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),  Wilaya ya Babati Vijijini Agatha Raphael amemshukuru Naibu Waziri kwa moyo wa kusaidia, akisema wema hauozi na wema ni akiba, huku akibainisha kuwa kitendo alichokifanya  ni cha mfano kinapaswa kuigwa na wengine.

Baadhi ya wazazi wenye watoto kutoka kundi hilo wamemshukuru Mhe.Ndege kwa msaada huo 

Wanawake wakiwa kwenye hafla hiyo

Wanawake wakiwa wamemtuza zawadi Mbunge wao Mhe. Ndege.
Mbunge Ndege akikabidhiwa zawadi ya mbuzi
Wakina mama wakiondoka na watoto wao kwa kutumia viti mwendo walivyokabidhiwa.
 

Post a Comment

0 Comments