Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe,akitoa maelekezo baada ya kutembelea kituo Cha Forodha cha Tarakea kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro kwa ya ziara ya kukagua shughuli zote za kibiashara zinazofanyika katika mipaka yote ya Mikoa ya kaskazini.
.........
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe Amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa mipakani ili mitaji yao ikue kutoka midogo kuwa katika wastani wa wafanyabiashara wakubwa.
Mhe. Kigahe ameyasema hayo leo septemba ,2024 alipokuwa akiongea na menejimenti ya wafanayakazi wa kituo Cha forodha cha Tarakea na wawakilishi wa wafanyabiashara wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Aidha mesema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara lengo lake ni kuwafanya wafanyabiashara wetu waweze kuuza bidhaa za mwisho watoke kwenye utaratibu wa kuuza Mazao na malighafi
Ameeleza kuwa Elimu ya ulipaji kodi iendelee kutolewa maafisa wa TRA ili kutanua wigo wa ulipaji kodi kusudi fedha itakayokusanywa iweze kuleta Maendeleo ikiwemo barabara,hospitali,shule na Masoko.
Nae Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro Bw.James Jilala ameeleze kuwa Tarekea ni moja ya vituo vinavyokua kwa kasi sana katika kuchangia mapato ya Serikali.
Kwa upande wake Alexander Mpwagi Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Tarakea ,akisoma taarifa ya utekelezaji wa kituo hicho ,amesema kuwa kituo kina ujumla wake kina watumishi 14 wanaotoka katika taasisi tofauti tofauti.
Kuhusu makusanyo ya mapato ya forodha ameeleza kuwa Mwaka 2023-2024 lengo likuwa kukusanya 24.5 Bilioni , makusanyo halisi yaliyopatikana ni 22.Bilioni
Aidha kwa mwaka 2024 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti kiasi Cha Shilingi 16.4 zimekusanywa.
Amezitaja bidhaa zinazoingia katika mpaka wa Tarakea kutoka nchi jirani ya Kenya ni Sabuni,Chewing gum,Margarine,Pipi na Food grade.
Kwa upande wa bidhaa zinazosafirshwa kutoka Tanzania kwenda Kenya kupitia mpaka wa Tarakea ni Makaa ya Mawe,Liquilified Petroleum gas,na bidhaa za mazo kama machungwa,Vitunguu,maji,Karanga,Viazi, na Mahindi.
Nae Katibu wa wafanya Biashara Wilaya ya Rombo Bw. Joseph Masika ameeleza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Biashara kutokuwa na magahala ya kuhifadhia mazao pindi wanapomaliza kuyavuna shambani.
0 Comments