Abbas Ali Mwinyi enzi za uhai wake
..............................
Na Dotto Mwaibale
MAMIA ya waombolezaji walijitokeza kwa wingi kumzika Abbas Mwinyi, mtoto wa aliyekuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, Hayati Ali Hassan Mwinyi, na kaka wa Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Abbas
alifariki usiku wa kuamkia Septemba 25, 2025 katika Hospitali ya Mkoa wa
Lumumba na mazishi yake kufanyika Septemba 26 katika makaburi ya familia Mangapwani.
Viongozi
mbalimbali wakiwepo wa dini wananchi ndugu, jamaa na marafiki walihudhuria
mazishi yake huku mitaa ya Unguja ikikugubikwa na huzuni wakati jeneza
lilipobeba mwili wake likiwa limebebwa kutoka Msikiti wa Zinjibar.
Mufti
Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaab, ndiye aliyewaongoza waumini kwenye
sala ya jeneza. Kisha, kwa heshima ya kitaifa, Mufti Mkuu wa Tanzania, Dk
Abubakar Zubeir, aliongoza sala ya mazishi Mangapwani.
Wananchi
walimwelezea Abbas kuwa alikuwa ni mtu mpole, mnyenyekevu, asiye na majivuno licha
ya hadhi ya familia yake huku baadhi yao wakisema hakutumia jina la baba yake wala nafasi ya
mdogo wake kama ngao ya majivuno, bali alijijengea heshima yake kwa unyenyekevu
na upendo kwa watu.
Abbas
ambaye alikuwa ni rubani mstaafu aliingia kwenye siasa mwaka 2020 na
kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Fuoni na kupitia nafasi yake hiyo aliwatumikia
wananchi kwa weledi mkubwa.
Abbas ndugu yetu mwendo
umeumaliza kapumzike kwa Amani utakumbukwa kwa mengi.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Abbas Mwinyi wakati wa mazishi yake
Mazishi ya Abbas Mwinyi yakifanyika
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Mjane wa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kufuatia msiba huo.
0 Comments