Subscribe Us

VIJANA WA KIUME WAANDALIWA SEMINA MAALUMU JIJINI DAR ES SALAAM

 Vijana wakiwa katika moja ya mikutano yao

..............................................

Na Mwandishi Wetu

 

HUDUMA ya Boys Revival Ministry (BOREMI) ya jijini Dar es Salaam imeandaa Semina maalumu kwa ajili ya vijana wa kiume. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Semina hiyo, Getrude Kilyabusebu alisema semina hiyo imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kundi hilo la vijana ambalo linaonesha kusahulika na badala yake yake kuangaliwa zaidi wasichana. 

“Kwa kulitambua jambo hilo kupitia ya Huduma ya Boys Revival Ministry (BOREMI) tukaone tuandae semina hii kwa ajili ya kuwapa mafunzo mbalimbali itakayowasaidia kuwaongezea uelewa katika maisha yao ili wawezi kuishi na jamii pasipo kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa,” alisema Kilyabusebu. 

Aidha, Kilyabusebu alisema mafunzo hayo yatatolewa na watoa mada wabobezi katika masuala ya makuzi ya vijana. 

Akinukuu kifungu cha biblia kutoka kitabu cha Ezekiel 4423, Kilyabusebu alisema ‘ Tuwafundishe kupambanua’ 

Mratibu huyo alisema Semina hiyo itafanyika Saa 7: 00 Mchana hadi Saa 12: jioni Hoteli ya AFCON 2027 iliyopo Mkabala na Mlimani City na vijana watakaoshiriki ni kuanzia umri wa  miaka 12 na kuwa hakuna kiingilio na chakula kitakuwepo. 

Kwa maelezo zaidi kuhusu semina hiyo namba ya mawasiliano ni +255 717 920 416 /*255 768 373 257Vijana wakionesha upendo wa kuwa katika picha ya pamoja

Post a Comment

0 Comments