..................................
Na Dotto Mwaibale
MHANDISI Kwilasa Deogratias Ntare anaomba ridhaa ya kupitishwa
na chama chake ili aweze kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) akishindana na Mbunge aliyemaliza muda
wake Stanslaus Mabula ambaye anatetea nafasi yake.
Ntare anakuwa ni mmoja wa makada wa chama hicho 26 watakaochuana na mbunge huyo aliye maliza muda wake anaye wania kipindi kingine cha tatu tangu alipo chaguliwa mwaka 2015 kushika nafasi hiyo.
Mmoja
wa watia nia wa nafasi hiyo atakaye chaguliwa na chama hicho na kushinda kwenye
uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu atakwenda kuwahudumia wananchi wa
kata 18 zilizopo katika jimbo hilo ambazo ni Lwanhima, Buhongwa , Mkolani, Luchelele, Nyegezi,
Butimba, Mkuyuni na Igogo.
Kata nyingine ni Pamba, Nyamagana, Milongo, Mbugani, Mahina,
Mhandu, Igoma, Mabatini, Kishili na Isamilo .
Ntare anatajwa kuwa ni mtia nia mwenye uzoefu wa masuala ya siasa kwani
nafasi yake katika chama hicho ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Goba, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akiwakilisha tawi
la Kitongwa, Mjumbe wa Kamati ya Maadili tawi la Kitongwa na Mjumbe wa Kamati
ya Siasa tawi la Kitongwa.
Kada huyo mbali ya kuwa mbobezi wa wa siasa pia ni mtaalamu wa masuala ya biashara ni Afisa masoko, Msimamizi wa mahusiano kwenye kampuni ya madini, W
wakala
wa matangazo na ving'amuzi na mtaalamu wa kilimo.
Kwenye
jimbo hilo Serikali imefanya kazi kubwa chini ya Rais Samia kupitia mbunge aliyemaliza
muda wake Stanslaus Mabula, lakini kutokana na kuwepo kwa demokrasia ndio maana
watia nia wengi wamejitokeza ili atayefanikiwa kuwa mbunge aweze
kuendeleza maendeleo kwenye maeneo ambayo bado yana changamoto
mbalimbali.
Jimbo la Nyamagana linahitaji kupata kiongozi bora mwenye uwezo,
weledi, mbunifu, maono na msomi ambaye atawaunganisha wana Nyamagana kushiriki
kila jambo na kulifanya liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kutekeleza
kwa ufanisi ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025/ 2030.Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nyamagana, Deogratias Nakey (kushoto), akimkabidhi fomu Mhandisi Kwilasa Deogratias Ntare ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Nyamagana lililopo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Julai 1, 2025.
0 Comments