.......................................
Na Mwandishi Wetu, Manyara
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara ikiongozwa na Mwenyekiti wake Elizabeth Malley wameendelea na ziara ya kuvunja makundi ya ubunge na udiwani ambapo walitembelea kata ya Bonga na Singe.
Mwenyekiti aliwataka waliokuwa wagombea kuwa kitu kimoja na kuwaunga mkono wote walioteuliwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya ubunge na udiwani.
Aliwataka pia wana CCM kuendelea kushikamana kuelekea uchaguzi mkuu.
0 Comments