Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela (kulia) wakati wa mkutano wa kujadili utekelezaji wa mageuzi ya mfumo mkuu wa benki hiyo, hatua ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma, kuimarisha usalama wa miamala na kukuza uchumi. Mkutano huo ulihudhuriwa na Manaibu Gavana wa BOT, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa BOT na Benki ya CRDB.
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, akieleza kwamba mageuzi ya mfumo wake mkuu wa kibenki (core banking system) ni hatua ya kimkakati na yenye kuonyesha ukomavu wa sekta ya benki nchini. Pongezi hizo zimetolewa wakati wa mkutano maalum kati ya menejimenti ya Benki ya CRDB na BOT ambao pia ulihudhuriwa na Manaibu Gavana, na Wakurugenzi wa Benki Kuu.
Pongezi za BOT zinakuja siku chache baada ya jumuiya ya kimataifa kutoa pongezi kwa Benki ya CRDB kufuatia mageuzi ya kihistoria ya mfumo wake, mageuzi ya kimkakati yaliyolenga kuongeza ubora wa huduma, kuimarisha usalama wa miamala, na kupanua wigo wa huduma bunifu kwa wateja wake.
0 Comments