......................................
Na Mwandishi Wetu, Manyara
Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi jimbo la Babati Vijijini Daniel Baran Sillo ameahidi kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Magara iwapo watamchagua katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza Oktoba 10, 2025 na Wananchi wa Vijijini vya Moya na Manyara vilivyopo katika Kata ya Magara, Mgombea huyo amesema wananchi wanalo jukumu moja la kujitokeza kwa wingi Oktoba 29,2025 kupiga kura na kumchagua Dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge pamoja na Madiwani wa CCM ili waweze kutekeleza kwa vitendo azma ya CCM yakuwaletea maendeleo Wananchi wake.
Sillo amesema iwapo atapata tena ridhaa ya wananchi ataendelea kuomba serikali kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiikabili kata hiyo ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, ukosefu wa umeme kwa baadhi ya Vitongoji na ukosefu wa miundo mbinu bora ya barabara katika kata hiyo.
Mgombea huyo ambaye hana mpinzani kwenye jimbo hilo amesema vipaumbele vyake vyote vilivyopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM atahakikisha anavitekeleza na kuleta maendelo kwa wananchi wake.
Sillo ameendelea na kampeni zake za kunadi sera za chama cha mapinduzi CCM katika jimbo la Babati Vijijini na mpaka sasa ameshazifikia kata kumi na saba kati ya kata ishirini na tano za jimbo hilo.
0 Comments