Dotto
Mwaibale na Philemon Solomoni
SHULE ya Sekondari ya Dr. Ali Mohammed Shein iliyopo Kata ya Misughaa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imefanya mahafali ya 16 ya wahitimu wa kidato cha nne huku ikijivunia ongezeko la ufaulu kwa miaka minne mfululizo.
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma akizungumza kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Oktoba 2, 2025 wakati akitoa taarifa ya maendeleo alisema shule yao imeendelea kupandisha ufaulu mwaka hadi mwaka kwa miaka minne mfululizo jambo ambalo wanajivunia.
Alisema mwaka 2019 walifikia asilimia 94, 2020 asilimia 97, 2021 asilimia 100, 2022 asilimia 100, 2023 asilimia 96 na 2024 asilimia 96.
“Shule yetu haijashuka kiufaulu mwaka 2021 na 2022 imeweza kufaulisha kwa asilimia 100 kwa kidato cha nne hili ni jambo jema na la kupendeza hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa matokeo hayo kwani wanafunzi wameweza kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mbalimbali nchini,” alisema Maruma.
Akizungumzia miundombinu alisema walipata msaada wa fedha za Uviko 19 ambapo walijenga madarasa mawili na chumba kimoja cha darasa fedha kutoka Serikali Kuu pia waliwezeshwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha maabara na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo fedha zilizotokana na tozo.
Alisema mwaka wa fedha wa 2024/ 2025 walifanikiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa chini ya mradi wa SEQUIP na mwaka wa fedha wa 2025/ 2026 Serikali iliwapatia Sh. Milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha chumba kimoja cha maabara.
“Kwa haya hatuna budi kumshukuru aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Miraji Mtaturu, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mbalimbali tuliyoitekeleza kupitia kwao, “ alisema Maruma.
Alitaja baadhi ya changamoto kuwa ni upungufu wa nyumba za walimu hali inayowafanya kuishi katika mazingira magumu, hawana ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufanyia shughuli mbalimbali na samani za maktaba.
Alitaja changamoto nyingine kuwa hawana hosteli ya kutosha kukidhi haja ya wanafunzi wanaotakiwa kukaa shuleni hasa kwa kuzingatia mtawanyiko na jiografia ya kata yao ya Misughaa.
Mwalimu Muruma alitaja changamoto nyingine kuwa ni uchakavu wa madarasa, jengo la utawala na kufanyiwa ukarabati chumba kimoja cha darasa na kuwekewa mifumo wezeshi ili kiweze kutumika kama ‘ Computer Room’
Akizungumzia kuhusu michezo Mwalimu Maruma alisema wameanzisha kituo cha kuibua vipaji vya mpira wa miguu kinachojulikana kwa jina la Misughaa Sport Centre.
Aidha, Mwalimu Maruma akizungumzia juu ya chakula kwa ajili ya wanafunzi alishukuru ushirikiano wanaoutoa wazazi kwani wanachakula cha kutosha hivyo kuwafanya wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kupata masomo na kupunguza utoro.
Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Fr. Patric Myuku kutoka Jimbo Katoliki Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi hao wasidanganyike kwa kuelezwa kuwa watoto hao hawata kuwa na msaada wowote kwao.
“Msidanganyike wasaidieni watoto wenu kwa kuwasomesha watakuja kuwasaidia baadaye mtakapokuwa wazee na ninyi ni mashahidi familia zilizoteseka kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao zinatofauti na zile ambazo hazikufanya hivyo,” alisema Fr. Myuku.
Fr. Myuku aliwataka wazazi hao kuwa na msimamo na kushirikiana na watoto wao bila ya kuyumbayumba katika kuwasaidia.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Athumani Kitiku aliwataka wazazi hao kuwapenda watoto wao na kueleza kuwa dunia ya sasa elimu ni bora zaidi kuliko urithi wa ng’ombe.
“Mwaka jana nilipata tabu kubwa kutokana na kuwepo kwa utoro wa wanafunzi na baadhi yenu ninyi kutowapeleka watoto wenu shule hadi kufikia hatua ya kupelekana mahakamani kwa ajili ya watoto wenu,” alisema Kitiku.
Kitiku alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wazazi hao kuwa atakaye bainika mtoto wake hajapelekwa shule kwa uzembe na utoro hawatamvumilia watampeleka mahakani ili sheria ichukue mkondo wake.
Jesca Selemani akizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi wa wahitimu hao wakati akitoa nasaha aliwataka kuzingatia elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.
“Hebu mshikeni sana elimu ndiyo maisha yenu ya baadaye kwani hata maandiko ya dini yameeleza kuwa itafuteni elimu musimuache aende zake hivyo wanapaswa kuishika na kuizingatia kinyume na hapo dunia itawameza.
Aliwaomba wazazi kuwashauri watoto vizuri na kuwaombea wafanikiwe katika masomo yao ili waweze kunufaika nayo.
Mahafali hayo yalinogeshwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wahitimu hao na wanafunzi wa madarasa mengine kwa kuimba nyimbo, kugani mashairi, maigizo, ngoma za asili, maonesho ya ukakamavu kutoka kwa skauti pamoja na kuonesha shoo ya uvaaji wa mavazi ya wataalam kama mwalimu, daktari, viongozi wa dini, wakulima, wanasheria na wanamuziki.
Walimu wa shule hiyo wakishiriki maandamano ya ufunguzi wa mahafali hayo.
Vijana wa Skauti wakiongoza maandamano hayo.
Skauti wakimpigia saluti mgeni rasmi baada ya kuwasili shuleni hapo
Vijana wa Skauti wakimvika Skafu mgeni rasmi wa mahafali hayo Fr,Patric Myuku Mjumbe wa bodi ya shule hiyo kutoka Jimbo Katoliki Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma akisalimiana na mgeni rasmi Fr. Patric Myuku.
Mgeni rasmi Fr. Patric Myuku. akisalimiana na viongozi mbalimbali wa shule hiyo
Mgeni rasmi Fr. Patric Myuku. akisalimiana na walimu wa shule hiyo
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma akimuelekeza jambo mgeni rasmi Fr. Myuku kuhusu ujenzi wa bweni la wanafunzi ambalo lipo hatua ya msingi na kumuomba kusaidia ujenzi huo.
Muonekano wa msingi wa jengo hilo.
Muonekano wa jengo la maabara la shule hiyo.
Muonekano wa moja ya madarasa ya shule hiyo.
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma akizungumzia kilimo cha migomba iliyopandwa shuleni hapo kwa ajili ya chakula na kulifanya eneo la shule hiyo kuwa na mandhari nzuri.
Mgeni rasmi Fr. Patric Myuku, akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne, wazazi na wanafunzi wengine.
Mkuu wa shule hiyo, Jackson Maruma akitoa taarifa ya shule hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Athumani Kitiku, akizungumza.
Jesca Selemani akitoa nasaha kwa wahitimu hao kwa niaba ya wazazi.
Imamu wa Msikiti wa Kata ya Misughaa, Hamisi Ramadhani akiomba dua kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Mshereheshaji (MC), namba mbili Eva Peter, akionesha umahiri wa kunogesha mahafali hayo.
Mshereheshaji namba moja j umanne Maulid Idd (maarufu kwa jina la J4) akiwajibika.
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Gabriel akionesha umahiri wa kugani mashairi.
Brayan Amnaary akigani mistari ya massshairi katika mahafali hayo.
Wahitimu Fadhila Rashid na Getrude Basil wakisoma makala maalum iliyohusu maisha ya mgeni rasmi na mafanikio yake ya kikazi na maisha kwa ujumla.
Skauti wakionesha ukakamavu wao wakati wa mahafali hayo.
Kwaito likioneshwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi wakiwa meza meza kuu.
Wahitimu wakiwapongeza wazazi wao.
Wazazi wakiwapongeza watoto wao kwa kufikia hatua hiyo ya kuhitimu kidato cha nne.
Walimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
WWalimu wa shule hiyo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Walimu Naomi Richard, Neema Mwaya na Sara Mwafwimba wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wazazi wakishiriki mahafali hayo.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu wakiimba wimbo maalum wa kuaga. Wimbo huo umetungwa na Mwalimu Umrisali Jumanne.
Watoto nao wanaoishi jirani na shule hiyo walijumuika kwenye mahafali hayo
Taswira ya mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa na zawadi ya vyombo walivyonunua kwa ajili ya kuwapa walimu wao.
Walimu wakiserebuka huku wakiwa wameshika vyombo walivyo nunuliwa na wahitimu hao.
Walimu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyombo hivyo.
Wapiga picha wa kujitegemea wakichukua matukio mbalimbali ya mahafali hayo.
Picha za matukio mbalimbali zikipigwa.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiigiza igizo la kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Wahimu wakionesha onesho la la vazi la wanamuziki.
Madansa wakionesha umahiri wa kucheza.
Wanafunzi mashabiki wa timu ya Simba wakitoa burudani.
Burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wanyaturu ikichezwa na wanafunzi wa shule hiyo.
Walimu wakiselebuka kwenye mahafali hayo.
Mgeni rasmi Fr. Patric Myuku akiendesha harambee kwa ajili yaujenziwa Hosteli ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mkuu wa shule hiyo Jackson Maruma akiwa kwenyemahafali hayo.
Mkuu wa shule hiyo Jackson Maruma akimkabidhi cheti mgeni rasmi cha kushiriki mahafali hayo.
Mgeni rasmi akiwakabidhi vyeti wahitimu.
Vyeti vikikabidhiwa.
0 Comments