Subscribe Us

NABII MKUU DR. GEORDAVIE MZALENDO WA KWELI ANAYEJITOA KUSAIDIA JAMII

Kiongozi wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye Makao Makuu yake Kisongo mkoani Arusha Nabii Mkuu Dr. GeorDavie, akizungumza.

.................................. 

UZALENDO ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi na  mzalendo wa kweli wakati wote anaweka maslahi ya nchi yake na ya jamii mbele. 

Uzalendo unabeba dhana pana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia vyote vikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa. 

Katika Taifa la Tanzania kumekuwepo na wazalendo wengi, baadhi wamekwisha tangulia mbele za haki akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Edward Moringe Sokoine, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Hayati Bibi Titi Mohamed na wengine wengi. 

Leo napenda kumuongelea  Kiongozi wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye Makao Makuu yake Kisongo mkoani Arusha Nabii Mkuu Dr. GeorDavie  alivyo mzalendo wa kweli katika kujitoa kwake kusaidia jamii na shughuli mbalimbali za maendeleo. 

Dr. GeorDavie tumemuona jinsi anavyojitoa kusaidia makundi mbalimbali ya watu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi. 

Hebu tuziangazie kwa kifupi baadhi ya kazi chache kati ya nyingi ambazo amezifanya katika kusaidia jamii nchini hususani Mkoa wa Arusha. 

Moja ya msaada alioutoa ni wa Sh. Million 11.5 kwa ajili ya kuwsaidia watu 23 walioathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa mkoani Arusha. 

Waathirika wa mafuriko hayo kila mmoja alipatiwa Sh. 500,000 ambazo zilitolewa kwa ajili ya kununua chakula, magodoro na vyombo msaada ambao ulikabidhiwa na Balozi wa Nabii huyo Mtume Sekela Ntondolo. 

Msaada mwingine ambao aliutoa ni wa Sh. Milioni 10 kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho Faraja Orphance Children's Home kilichopo maeneo ya Kambi ya Chupa jijini Arusha. 

Aidha Dr. GeorDavie alitoa msaada wa Sh. Milioni 100 kwa wafanyabiashara wa Soko la Samunge kwa ajili ya kukuza mitaji yao. 

Katika matukio mengine Dr. GeorDavie alitoa Sh. Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Likamba iliyopo eneo la Kisongo barabara ambayo iliharibiwa na mvua za masika za mwaka jana. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngorbob, Mohamed Nassoro alisema Nabii huyo ametumia zaidi ya Sh. Milioni 116.5 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi wa maabara katika kijiji hicho. 

Msaada mwingine alioutoa ni Sh. Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa vitanda 20 katika Shule ya Sekondari ya Lepurko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Monduli. 

Hii ni baadhi tu ya misaada kati ya mingi ambayo ametoa fedha kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii jambo ambalo ni zuri kwani linachagiza maendeleo ya wananchi. 

Kutokana uzalendo wake kwa nchi pamoja na chama Tawala mapema wiki hii tumeshuhudia akikabidhi Sh. Milioni 50 kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha ili kuwesha kampeni za Mgombea Urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajia kuanza mikutano yake ya kampeni mwanzoni mwa mwezi oktoba mkoani humo. 

Akikabidhi fedha hizo Septemba 25, 2025 Makao Makuu ya Chama hicho Mkoa wa Arusha, Nabii Geor Davie alimueleza Katibu Mkuu wa CCM Mkoa, Musa Matoroka kuwa anajisikia fahari kuchangia chama chake na kumtakia kheri Dkt. Samia kwenye kampeni zake anazoendelea kuzifanya nchi nzima. 

“Nashukuru kwa fursa ya kuchangia chama chetu, hasa katika ujio tunaoutarajia wa Mwenyekiti wa chama chetu Taifa kuelekea uchaguzi Mkuu,” alisema Dr. GeorDavie. 

Kwa upande wake Matoroka kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha alimshukuru Nabii huyo kwa mchango wake huo wa hiari. 

Alisema Chama Cha Mapinduzi na serikali wanaunga mkono jitihada zake katika malezi ya kiroho kwa waumini wake pamoja na shughuli za maendeleo anazosaidia mkoani humo. 

Kiongozi wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye Makao Makuu yake Kisongo mkoani Arusha Nabii Mkuu Dr. GeorDavie, akihubiri katika moja ya ibada zake.
Kiongozi wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye Makao Makuu yake Kisongo mkoani Arusha Nabii Mkuu Dr. GeorDavie, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Samunge Arusha.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko la Machinga la Samunge wakifuatilia jambo Nabii Mkuu Geordevi Kasambale wa huduma ya Ngurumo ya Upako alipotembelea soko hilo.

Makala hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.
 

Post a Comment

0 Comments