Mzee Said Bakari Nyumbu (kulia) na Mzee Ally Abdallah Ngurungu wakazi wa Mtaa wa Ngurungu , Maji Matitu (A) Mbagala Jijini Dar es Salaam wakiwa pamoja. Wazee hawa wanasumbuliwa na maradhi wanaomba msaada wa matibabu.
..................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
WAZEE Said Bakari Nyumbu (68) na Mzee Ally Abdallah Ngurungu
(70) wakazi wa Mtaa wa Ngurungu , Maji
Matitu (A) Mbagala Jijini Dar es Salaam maisha yao yapo hatarini kufuatia
maradhi yanayo wasibu na sasa wanategemea kudra tu za Mwenyezi Mungu wanaomba msaada wa matibabu..
Awali Mzee Ngurungu licha ya kuwa na changamoto za kiafya ndiye aliyekuwa akimsaidia Mzee mwenzake Nyumbu ambaye
hana ndugu anaishi kwa kusaidiwa na wasamaria wema baada ya bosi wake aliyekuwa
akimsaidia kazi kushindwa kumsaidia kutokana na uzee.
Wazee hawa wanachangamoto ya maradhi ya utu uzima ambapo
Mzee Nyumbu anachangamoto ya usikivu
hafifu, Tezidume na anakidonda katika moja ya kidole chake ambacho kila siku
kimekuwa kikiongezeka na hivyo kumfanya akate tamaa ya kuishi.
Hivi sasa Mzee Nyumbu amelazwa Hospitali ya Rifaa ya Mkoa wa
Temeke ambapo bado hajaanza kupatiwa matibabu zaidi ya kupewa dawa za kutuliza
maumivu.
Kwa upande wa Mzee Ngurungu yeye anasumbuliwa na ugonjwa wa
kisukari, miguu kupata ganzi, uoni hafifu na mwili kukosa nguvu.
Mzee Ngurungu anasema ameshindwa kwenda hospitali kwa kuwa
hana fedha hivyo yupo tu nyumbani akiteseka kwa maumivu.
Ndugu watanzania hayo ndiyo madhira wanayopitia wazee wetu
hawa ambao mimi naweza kuwaita mapacha kutokana na ukaribu walionao ambao umewafanya
wafahamiane kutokana na changamoto walizonazo.
Wazee hawa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo za maradhi
pia wanachangamoto za mahitaji mengine ya kibinadamu kama chakula hivyo
wanaomba msaada wa kupata matibabu na mahitaji hayo mengine.
Kama mtaguswa kuwasaidia hata Shilingi 2000 utakayokuwa nayo
unaweza kuwasiliana na Mzee Ally Abdallah Ngurungu kwa namba ya simu 0784679755
au Mwandishi wa taarifa hii kupitia namba 0754362990 kwa maelezo zaidi.
Ndugu Watanzania kila mmoja kwa Imani yake wazee wetu hawa
wamekwama wanahitaji msaada kutoa ni
moyo wa mtu na wala siyo utajiri.
Changamoto za Wazee hawa zimeibuliwa na Wajumbe wa Serikali
ya Mtaa wa Matitu A ikiwa ni moja ya njia ya kutatua changamoto za wananchi
wajumbe hao ni Hawa Omari na Jihadi Umwagala.
Wazee hao wakiwa pamoja Maji Matitu (A) Mbagala Jijini Dar es Salaam.
0 Comments