Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Babati Mjini, Magdalena Urono akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakiomba kura za wagombea wa chama hicho. Kulia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini, Emmanuel Khambay na kushoto ni Katibu wa Hamasa wa wilaya hiyo, Haji Ally,
............................................
Na Mwandishi Wetu, Manyara
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya
Babati Mjini unaendelea kwa kasi kusaka kura za wagombea wa chama hicho katika
siku chache zilizobaki kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29,
2025.
Akizungumza wakati wakiomba kura leo Oktoba 16, 2025
mwenyekiti wa umoja huo Wilaya ya Babati Mjini, Magdalena Urono alisema kasi ya
kutafuta kura za wagombea wao imeongezeka ambapo wanapita kila kona walipowananchi
kuwaomba kura zao kwa ajili ya CCM.
“Tupo na mgombea wetu wa nafasi ya ubunge jimbo la Babati
mjini, Emmanuel Khambay tunapita kila kona walipo wananchi na makundi yaa
vijana kuzisaka kura za wagombea wetu wote wa CCM kwa kweli wanatuelewa na
wametuahidi kutupa kura, “ alisema Urono.
Alisema matamanio yao ni kuona wilaya hiyo inakuwa ya kwanza
kwa kuwa na kura nyingi za mgombea nafasi ya urais Dkt. Samia Suluhu Hassan,
mbunge na madiwani.
Alisema wanazisaka kura huku wakielezea kazi kubwa
iliyofanywa na Serikali kupitia ilani ya CCM ya 2020/ 2025 chini ya Mwenyekiti
wa Taifa wa chama hicho Dkt. Samia kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Mgombea ubunge wa jimbo hilo Emmanuel Khambay aliwaomba
wananchi hao kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura za wagombea wa CCM na
kueleza kuwa ndiyo chama pekee ambacho kimebeba maono ya maendeleo.
“Tuchagueni wagombea wote wa CCM kwani ndiyo chama chenye
mipango mizuri ambayo inaenda kutekelezwa katika ilani ya uchaguzi ya 2025/
2030,” alisema Khambay.
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Babati Mjini, Emmanuel Khambay, akizungumza wakati akiomba kura.
Salamu zikitolewa kabla ya kuomba kura. Kutoka kulia ni Katibu Hamasa wa wilaya hiyo, Haji Ally, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Emmanuel Khambay, Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo, Magdalena Orono na kada wa chama hicho.
Kura zikiombwa kwa wananchi (hawapo pichani)
0 Comments