..................................
Alisema Serikali imekuwa ikipokea fedha kutoka kwenye Mifuko ya Kimataifa ya
Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF)
na Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi (GCF).
"Fedha hizo zinazotolewa zimekuwa zikitumika katika kutekeleza miradi
mbalimbali ya hifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika pande zote
mbili za Muungano na kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutekeleza Mradi wa Kurejesha
Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula kwenye maeneo mbalimbali
nchini" alisema Khamis.
0 Comments