Akızungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea Urais kupitia CCM Dk.Samia Suluhu Hassan uliofanyika wilayani Pangani mkoani Tanga,Nape amesema walipompitisha Dk.Samia Chama kilifanya tathmini ya kina wakajirishisha anatosha, ni mzalendo na ana uwezo lakini ni muumini thabiti wa utu wa binadamu ndiyo maana wamempeleka kwa Watanzania kuomba ridhaa.
“Nitatoa mifano michache kuthibitisha uwezo wake Rais Dk.Samia alipoingia madarakani aliingia wakati nchi yetu imepata msiba na alikuta miradi mikubwa inaendelea siyo tu miradi hiyo imeendelea lakini miradi mingi ameikamilisha mingine inaendelea vizuri lakini akaanzisha na miradi mingine ya ujenzi ya ziada.
“Sisi CCM tathmini yetu ikatuonyesha siyo tu kwa sababu ya utamaduni ni kwa sababu ameweza na ndiyo maana tukasema tunaendelea naye. Mama Samia ameikuta nchi yetu inakusanya kwa mwaka trilioni 18 kwa usimamizi mzuri kwa uzalendo mzuri amesimamia tumefikisha trilioni 32.
“Hizo fedha ndizo hizo ambazo mmeziona zimekuja kwenye maji, barabara, afya, ajira na wote walioguswa na fedha hii tarehe 29 tunakazi moja ya kutiki,”amesema Nape .
Akieleza zaidi amesema Dk.Samia alipoingia madarakani alikuta Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali ilikuwa inafanya ukaguzi katika maeneo ya ofisi yasiyozidi 900.
“Hati zilikuwa kidogo zinasumbua Mama alipoingia madarakani kwa sababu ya usimamizi wake kusimamia mapato na kudhibiti mapato ya serikali akaagiza ba kuongezeka maeneo ya ukaguzi kutoka 900 hadi 1300.
“Ukaguzi wa mwisho uliofanyika maana wapo wanaopotosha ripoti ya CAG, katika hati 1300 asilimia 99 ni hatuli safu. Anayesema Samia hakuweza yuko wapi.Ungekuwa wewe ungemteua kuwa mgombea. Amesimamia mapatio yameonekana, amedhibiti matumizi na ndiyo maana asilimia zimeongezeka.
“Lakini tukajiridhisha kwamba mama huyu ni muumini wa utu wa binaadamu na hapa nitoe mifano michache.Tunazosheria zinazosimamia haki jinai ukienda polisi, mahakamani na vyimbo mbalimbali tumekuwa nazo kwa miaka 60 toka tulipopata uhuru.”
Ameongeza baadhi ya sheria zimeguswa na nyingine baadhi zinerekebishwa lakini mama kwa sababu ya uumini wa utu wa binadaamu aliamua kuunda tume ya Rais kwa lengo la kushughulikia haki jinai.
“Tume ikaleta ripoti na matokeo tumeanza kuyaona huo kama sio utu ni nini? Hata ungekuwa wewe mjumbe wa mkutano mkuu, mjumbe wa halmashauri kuu ungekipitisha chuma hiki kikasimamie haki.”
Pia amesema kuwa Dk.Samia alipoingia madarakani aliwakuta akinamama katika vizazi hai 100,000 vizazi hai 556 vinakufa lakini akawatoa kutoka 556 hadi 114. “Alafu leo useme tarehe 29 usiende kutiki. Watu wanajua, wanaenda kutiki kwa utu wa mama huyu.”
Nape amesema pia Dk.Samia wakati anaingia madarakani amekuta hasa kinamama walikuwa wanatumia mkaa na kuni, maisha yao yalikuwa hatarini hivyo akaanzisha kampeni ya nishati safi kupikia.
“Akatutoa kutoka asilimia sita mpaka leo tumefikia asilimia 20 na dunia imekubali, Afrika imekubali.Wewe mshamba usiyetaka kukubali hivi umechanganyikiwa au unataka kujikoroga mwenyewe
“Nimesimama kuwathibitishieni huyu mama (Dk.Samia) kazi anaiweza takwimu hazidanganyi zipo mezani. Wanaobisha wapingane na hizi takwimu kwamba hajapandisha mapato au hajapandisha.
“Kwamba hajisimamia matumizi ya fedha au amesimamia ?Ripoti ya mkaguzi inathibitisha kwamba ana utu na nimetoa mifano michache kuthibitisha.Kama mtu yupo tayari kuokoa roho za kinamama na watoto waliokuwa wanapotea kama siyo utu ni nini?”
0 Comments