Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Kibamba, jijini Dar es Salaam Mhe. Kairuki amesema atashirikiana na Mamlaka ya Uthibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuanzisha ruti ya moja kwa moja ya Kibamba hadi Kariakoo kwa Lengo la kurahisisha usafiri kwa wananchi na kupunguza gharama za kusafiri.
Mbali na hilo, Kairuki ameahidi kusimamia uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kupitia upatikanaji wa maeneo rasmi ya biashara na kuangalia uwezekano wa kuanzisha soko la kisasa litakalosaidia kuinua kipato cha wakazi wa eneo hilo na kuendeleza shughuli za kibiashara kwa ufanisi na bora.
Mgombea huyo amewahimiza wananchi wa Kibamba kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29 kwa kuwa uchaguzi huo ni fursa ya kuendeleza jitihada za maendeleo katika jimbo hilo kwa kuchagua wagombea wa CCM katika nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.
Kairuki ameahidi kuwa, iwapo atachaguliwa, kipaumbele chake kitakuwa ni kuhakikisha wananchi wanapata usafiri wa uhakika, biashara zinakuwa, na maendeleo yanashikilia kasi, ili Kibamba iwe eneo lenye ustawi na fursa za kiuchumi kwa wote.
0 Comments