Subscribe Us

STANBIC YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH. MIL. 60 KWA HOSPITALI YA TUMBI

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wateja Maalumu wa Benki ya Stanbic, Omari Mtiga (mwenye fulana ya bluu), akipeana mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Dkt. Amani Malima, wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 kutoka Benki ya Stanbic, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja na pia ya maadhimisho ya Miaka 30 ya benki hiyo tangu ianze kutoa huduma nchini.
........................................

Pwani, Oktoba 10, 2025 — Benki ya Stanbic imekabidhi msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni 60 kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuboresha huduma za afya nchini.

Msaada huo, unaojumuisha kompyuta, vitanda, viti vya wagonjwa (wheelchairs), matoroli, na vifaa vya usafi, ulikabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wateja Maalumu wa Stanbic Bank, Bw. Omari Mtiga, kwa niaba ya benki hiyo, na kupokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Dk. Amani Malima.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano, Bw. Mtiga alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango endelevu wa uwajibikaji wa kijamii (CSR) wa Stanbic Bank, unaolenga kurudisha fadhila kwa jamii, sambamba na maadhimisho ya Miaka 30 ya Kukua Pamoja tangu benki hiyo ianze kutoa huduma nchini Tanzania.

Tunatambua mchango mkubwa wa sekta ya afya katika ustawi wa jamii. Kupitia msaada huu, tunalenga kusaidia hospitali kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa na kuongeza ufanisi wa watoa huduma. Hii ni moja ya njia tunazosherehekea miaka 30 ya kukua pamoja na Watanzania,” alisema Bw. Mtiga.

Post a Comment

0 Comments