Subscribe Us

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI BINAFSI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Skauti wakimvika Skafu Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi alipomwakilisha Waziri wa Afya Mhe Mohamed Mchengerwa katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph yaliyofanyika Juni 13, 2026 mkoani Kilimanjaro.

........................................

Na Shaban Juma, Kilimanjaro

Serikali imeihakikishia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph, Moshi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha huduma za afya pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili hospitali hiyo kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi (Mb), akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Mohamed Mchengerwa katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph yaliyofanyika Juni 13, 2026 mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Samizi amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali katika utekelezaji wa sera na mipango ya sekta ya afya, hali iliyopelekea kukua kwake kutoka kituo cha afya hadi kuwa hospitali ya rufaa ya mkoa inayohudumia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani.

Aidha, amesema Serikali kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) itaendelea kuimarisha ushirikiano na hospitali binafsi na za dini ili kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya, kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi na kuhakikisha rasilimali za sekta ya afya zinatumika kwa ufanisi.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana kwa karibu na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph kwa kuhakikisha inaendelea kugharamia mishahara ya watumishi, dawa na vifaa tiba ili kuimarisha huduma kwa wananchi,” amesema Dkt. Samizi.

Pia amesema Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha hospitali nchini zinapata ithibati ya kimataifa (International Accreditation) ili huduma zinazotolewa zikidhi viwango vya kimataifa na kusaidia kukuza tiba utalii nchini sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.

Akizungumzia changamoto zilizowasilishwa na hospitali hiyo, Dkt. Samizi amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph katika kutafuta suluhisho la changamoto ikiwemo uhaba wa watumishi wa kada mbalimbali, ukosefu wa fedha pamoja na hitaji la mashine ya CT-Scan.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi (Mb), akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili kwenye kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph yaliyofanyika Juni 13, 2026 mkoani Kilimanjaro.

Matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.










Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi (Mb), akizungumza na wagonjwa alipowatembelea  katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa St. Joseph yaliyofanyika Juni 13, 202

Post a Comment

0 Comments