WALIMU Wanachama wa Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) wamelalamikia kitendo cha baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanaohamia kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuzuiwa kujiunga na chama hicho ambacho kipo kwa mujibu wa sheria.
Wanaotuhumiwa kuwazuia walimu hao ni Wakurugenzi, Maafisa Utumishi Wakuu na Maafisa
Utumishi Wasaidizi wa Halmashauri mbalimbali nchini.
Walimu hao
wanadai kuwa licha ya kujiunga na CHAKAMWATA kwa kufuata hatua zote za
kisheria, Maafisa hao wanaoingia kwenye mfumo wa mishahara yao (LAWSON) na wamekuwa wakikataa kuwaunga CHAKAMWATA walikojiunga badala yake
wanawalazimisha wabaki CWT walikojitoa.
Maafisa hao wanadaiwa kukataa kuondoa makato ya 2% ya CWT na kuingiza michango ya 1% ya CHAKAMWATA kwenye mishahara ya Walimu wanaojitoa kutoka CWT na kujiunga na CHAKAMWATA.
KUENDELEA KUSOMA




0 Comments