
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, alisema uzinduzi huo ni ushahidi wa safari endelevu ya kampuni hiyo katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za nishati zilizo bora, za uhakika, nafuu, na zinazopatikana karibu na makazi na shughuli zao za kila siku.
“Puma Energy Tanzania imejikita katika dhamira ya msingi ya kuwawezesha wananchi. Kituo hiki kipya ni kielelezo halisi cha dhamira hiyo, kikiwa kimejengwa mahsusi kuhudumia wakazi wa maeneo haya, wafanyabiashara, na wasafiri wanaotumia barabara hii muhimu kwa kuwapatia huduma bora, salama na za kisasa zinazorahisisha maisha yao ya kila siku,” alisema Bi. Abdallah.
Alibainisha kuwa uwekezaji huo hauhusiani tu na huduma za mafuta, bali unalenga kutoa huduma jumuishi. Kupitia kituo hicho kipya, kampuni imeweza kutoa ajira kwa zaidi ya watu 23, hivyo kuchangia moja kwa moja katika uchumi wa ndani na ustawi wa jamii inayowazunguka.
Mbali na huduma za mafuta, kituo hicho kinajumuisha:
- Duka la rejareja lenye bidhaa za kila siku,
- Duka la dawa (famasia), na
- Karakana ya kisasa kwa ukaguzi na matengenezo ya magari.
Bi. Abdallah aliongeza kuwa Puma Energy Tanzania inaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha huduma za nishati zinapatikana kwa urahisi, ubora, na usalama.
“Kila kituo kipya tunachokifungua ni zaidi ya jengo au pampu ya mafuta — ni uwekezaji katika maisha ya Watanzania na katika mustakabali wa taifa letu,” alisisitiza.
0 Comments