Subscribe Us

SANLAMALLIANZ YAUNGA MKONO SAFARI YA ALOYCE SIMBU KUELEKEA SANLAM CAPE TOWN MARATHON

Dar es Salaam, 16 Oktoba 2025 

Kampuni ya bima za maisha SanlamAllianz Life Insurance imekutana na mwanariadha nyota wa kimataifa Aloyce Simbu na kumkabidhi bendera ya Taifa kama ishara ya kumtakia kila la heri katika ushiriki wake kwenye Sanlam Cape Town Marathon, itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii nchini Afrika Kusini.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za SanlamAllianz jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa SanlamAllianz, Bw. Kyenekiki Kyando, alisema kuwa imekuwa ni desturi ya kampuni hiyo kuwaunga mkono wanariadha wanaofanya vizuri kwenye mbio za CRDB na NBC Marathon, kwa kuwapeleka kushiriki katika Sanlam Cape Town Marathon kama njia ya kuwaongezea uzoefu wa kimataifa na kuhamasisha michezo nchini.

SanlamAllianz inaamini katika kukuza vipaji vya michezo na kutoa fursa kwa wanariadha wetu kupata uzoefu wa kimataifa. Huu ni mwendelezo wa jitihada zetu za kuunga mkono afya njema, ustawi na michezo kupitia programu mbalimbali za kijamii,” alisema Bw. Kyando.

Kwa upande wake, Aloyce Simbu alishukuru SanlamAllianz kwa msaada na imani waliyoonesha kwake, akieleza kuwa amejiandaa vyema na yuko tayari kupeperusha bendera ya Tanzania katika mbio hizo maarufu za kimataifa.

Ninashukuru SanlamAllianz kwa kuniunga mkono. Nitajitahidi kufanya vizuri ili kuiwakilisha vyema Tanzania na kuongeza heshima kwa taifa letu,” alisema Simbu.SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments