........................................
Na Mwandishi Wetu, Mara
Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Vyuo na vyuo Vikuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Emanuel Martine Oktoba 14, 2025 amekutana kuzungumza na wapiga kura wa mara ya kwanza Samia First Time Voters ambao walikuwa katika kambi ya michezo ya ndondo CUP Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.
Vijana wapiga kura wa Mara ya kwanza ndani ya Mkoa wa Mara wameahidi kujitokeza kwa wingi kwenda kumpa kura Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na maendeleo mengi yaliotekelezwa na Serikali ya nchini
Martine akiwa mkoani humo amemuombea Kura Dkt Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani wanaotokana na CCM.
0 Comments