Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelok Sokoine, akiwahutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jimbo la Hanang' uliofanyika Septemba 16, 2025.
.............................................
Na Mwandishi Wetu, Hanang'
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelok Sokoine, amezindua rasmi kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Hanang’ na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29 mwaka huu kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kata ya Gehandu, Namelok alisema wananchi wa Hanang’ wamepata “redio ya kimataifa” kupitia mgombea ubunge wa CCM, Asia Abdulkarim Halamga, ambaye atawapigania bila kuchoka bungeni na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi.
“Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika kipindi cha miaka minne, tumpe kura aendelee kuleta maendeleo zaidi. Wana Hanang’ mmechagua redio, na kazi yangu ni kuchukua habari zenu na kuzifikisha panapohusika. Nitahakikisha serikali inapata fedha lakini wananchi .hawaumii,” alisema Namelok.
Katika mkutano huo, Namelok alimmnadi mgombea ubunge Asia Halamga pamoja na madiwani wote wa kata 33 za Jimbo la Hanang’, akisisitiza kuwa CCM imejipanga kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, barabara na umeme.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima, alisema chama kimejipanga kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kikubwa kwenye uchaguzi mkuu, na kuwataka wananchi waendelee kuiamini CCM kama chama pekee chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli.
Uzinduzi huo ulifanyika kwa shamrashamra kubwa, ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria na kuonyesha hamasa ya kuunga mkono wagombea wa CCM.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelok Sokoine, akiwanadi mgombea nafasi ya Ubunge wa Jimb la Hanang' Asia Abdulkarim Halamga na Diwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo hilo uliofanyika Septemba 16, 2025.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima, akizungumza kwenye uzinduzi huo.Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
0 Comments