Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali, ambaye alikuwa mgeni rasmi akisisitiza jambo wakati akifungua Semina ya Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) na Mawakala wa Huduma za Fedha wa Wilayani humo iliyofanyika Oktoba 22, 2025
.........................................
Na
Dotto Mwaibale, Mkalama
MKUU wa Wilaya ya
Mkalama mkoani Singida Mhe. Moses Machali, ameipongeza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa
Singida kwa jinsi ilivyojidhatiti kukabiliana na vitendo vya rushwa.
Machali
alitoa pongezi hizo Oktoba 22, 2025 wakati alipokuwa akifungua Semina ya Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) na Mawakala wa Huduma za Fedha
Wilaya ya Mkalama iliyofanyika Oktoba 22, 2025.
“
Nikiwa kama kiongozi wa Serikali kwa mujibu wa sheria napenda nitumie fursa hii
kuupongeza uongozi mzima wa TAKUKURU kuanzia Mkoa na katika wilaya chini ya
Mkuu wa Takukuru mkoa Sosthenes Kibwengo kwa kazi nzuri mnayoifanya ya
kukabiliana na vitendo vya rushwa,” alisema Mhe. Machali.
Machali
alisema hana tabia ya kumsifia mtu lakini pale anapofanya vizuri hasiti kufanya
hivyo kwani wanafanya kazi kubwa na nzuri ya kuelimisha wananchi dhidi ya
rushwa.
Aidha,
Machali kwa niaba ya Serikali alitumia nafasi hiyo kuwapongeza maafisa
usafirishaji (Bodaboda) na Mawakala wa Huduma za Fedha kwa kukubali mualiko wa
TAKUKURU kwenda kuhudhuria semina hiyo ili waweze kuelimishana juu ya mapambano
ya masuala rushwa.
Pamoja
na mambo mengine Semina hiyo iliyoandaliwa na TAKUKURU Wilaya ya Mkalama imelenga kuongeza uelewa kuhusu uwajibikaji, uwazi
na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa katika sekta ya usafirishaji
(bodaboda) na kwa watoa huduma za kifedha hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali, akizungumza kwenye Semina hiyo.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Nduguti Mrakibu Msaidizi (ASP) Fedrick Magowa akizungumza na maafisa Usafirishaji na Mawakala wa Huduma za Fedha..
Semina ikiendelea
Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wakiwa kwenye Semina hiyo.








0 Comments