HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa makosa binafsi yameigharimu timu kupoteza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Iran 2-0 Tanzania, mabao yakifungwa na Amirhossen Hosseinzadeh dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti na Mohammad Mohebi dakika ya 26.
Morocco amesema kuwa walianza kwa kutengeneza nafasi kupitia kwa kiungo Feisal Salum lakini alikosa kufunga mwisho wapinzani wakapata nafasi wakatumia.
“Tulikuwa na mchezo mgumu na mapema tulipata nafasi tukashindwa kutumia. Makosa ya mtu mmojammoja yalitokea na hapo wapinzani wetu wakapata nafasi wakatumia.
“Kipindi cha pili tulikuwa imara lakini tulishindwa kutumka nafasi ambazo tulitengeneza. Wapinzani walitupa presha kubwa ilikuwa hivyo lakini ni matokeo ya mpira, “..SOMA ZAIDI
0 Comments