Baadhi ya washiriki wa maandamano katika kilele cha siku ya afya ya akili duniani. ................................. Na Mwandishi Wetu, Manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Manyara ni sehemu moja wapo ambayo inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa afya ya akili kwani matukio ya kikatili, kujidhuru na kudhuru wengine yamekithiri .
Sendiga amesema hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Manyara katika viwanja vya moteli papaa.
Amesema madhara hayo yamekuwa yakisababishwa na mawazo, matumizi makubwa ya madawa ya kulevya, ukatili wa kijinsia, kipato duni na ukosefu wa ajira, lishe duni, utapiamlo na udumavu licha ya kuwa ni mkoa unaozalisha kwa wingi mazao aina zote ya chakula.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Queen Sendiga akizungumza. Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema ni vyema kuhakikisha wenye maradhi hayo wanafikishwa mapeka katika Hospitali hiyo, huku akielezea namna walivyojipanga katika kuboresha huduma za afya ya akili katika Mikoa na Taifa kwa ujumla.Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema ni vyema kuhakikisha wenye maradhi hayo wanafikishwa mapeka katika Hospitali hiyo, huku akielezea namna walivyojipanga katika kuboresha huduma za afya ya akili katika Mikoa na Taifa kwa ujumla.
0 Comments