.......................................
Na Mwandishi Wetu, Hanang'
Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Hanang zimefungwa rasmi Oktoba 25, 2025 katika mkutano uliofanyika Bassotu, ukiongozwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM Kanda ya Kaskazini, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ukihudhuriwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hanang, kupitia CCM, Asia Halamga.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
Katika ufungaji wa kampeni hizo Sumaye alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na ushiriki wa wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 na kuwaomba kujitokeza kwa wingi kwenda kuwapigia kura wagombea wa CCM ambao ni Mgombea Urais, Ubunge na Diwani.




0 Comments