Washiriki wa Maonesho ya Mat Contractors wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Mzee Peter Mavunde (katikati aliyevaa kofia) ambaye alikuwa mgeni rasmi.
....................................
Na
Godwin Myovela, Dodoma
Maonesho
ya wakandarasi na usambazaji wa vifaa vya ujenzi chini ya uratibu wa Mat
Builders and Contractors Global Expo (Goal 2050) yameendelea kutawala anga ya
viwanja vya Nyerere Square, Dodoma, yakionesha dira mpya ya ukuaji wa sekta ya
ujenzi, uchumi na teknolojia nchini.
Mwenyekiti
wa maonesho hayo, George Mandila, amesema maonesho haya ni mara ya pili
kufanyika Dodoma na mara ya saba mfululizo nchini tangu kuanzishwa mwaka 2024,
na mwaka huu yameonesha mafanikio makubwa kuliko yote yaliyowahi kufanyika.
Akizungumza
mbele ya wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi, Mandila alifafanua kuwa mafanikio
ya maonesho haya yametokana na ushawishi na ubunifu mkubwa uliowezesha ushiriki
mpana wa makampuni makubwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema
ushiriki wa nchi kama China na Jamhuri ya Czech, sambamba na taasisi na
mashirika makubwa ya Stamico, Samsung, pamoja na taasisi muhimu za masoko ya
mitaji ikiwemo UTT AMIS umeibua matumaini mapya kuhusu mchango mkubwa wa sekta
ya ujenzi katika kukuza uchumi wa taifa kabla ya 2050.
"Maonesho
haya yamegeuka jukwaa la teknolojia bunifu, yakiweka wazi bidhaa na mitambo ya
kisasa ikiwa ni pamoja na makontena ya kawaida na ya jokofu, mashine za
kuchimba madini na teknolojia za umwagiliaji," alisema Mandila na
kuongeza;
Pia
tuna magari ya ujenzi, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya kuchakata mazao kama
alizeti, asali na nafaka, pamoja na mashine za kuongeza thamani katika sekta ya
kilimo, ujenzi na madini.
Idadi
kubwa ya wananchi, wajasiriamali, wataalamu wa sekta ya ujenzi na wawekezaji
imejitokeza, ikionesha kiu kubwa ya kuchangamkia fursa na ushirikiano wa
kimkakati.
Kwa
mujibu wa Mandila, dhima kuu ya Mat Global Expo (Goal 2050) ni kusisimua uchumi
wa kila mkoa unaofikiwa, kupitia uwezeshaji wa watu katika uzalishaji, ajira,
ubunifu, na matumizi ya teknolojia.
“Mtu
mmoja akinunua lori la mchanga au mashine ya kukamua alizeti, hawezi kunufaika
peke yake; hapo mama lishe atapata kazi, bodaboda atabeba mizigo, gesi itauzwa,
vijana wataajiriwa, na mitaa itachemka kiuchumi,” alisema kwa msisitizo.
Mandila
anaongeza kuwa, maonesho haya ni zaidi ya biashara. Ni majukwaa ya
kufungamanisha uchumi wa viwanda, ujenzi, kilimo, madini, TEHAMA na sera za
uwekezaji wa kimataifa.
Yanatoa
nafasi za kujifunza, kujenga ushirikiano wa kimkakati, kuzalisha ajira, na
kuandaa taifa kuelekea uchumi imara, jumuishi na shindani ifikapo mwaka 2050.
Katika
viwanja vya Nyerere Square, makampuni makubwa yanaonesha mitambo mikubwa yenye
uwezo wa kuchimba, kuchakata na kuzalisha kwa viwango vya kimataifa.
Washiriki wamekuwa wakitoa elimu kuhusu namna ya kufadhili miradi ya wakandarasi, wajasiriamali na wawekezaji wadogo na wa kati kwa urahisi na usalama jambo lililoonesha kuvutia vijana na wanawake kwa makundi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akipata maelezo alipotembela mabanda katika maonesho hayo.






0 Comments