Subscribe Us

DKT. NUWAS AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Dkt Emanuel Nuwas akishiriki kupata chakula na watu wenye mahitaji maalumu baada ya kufanyanao kikao Desemba 24, 2025.
..................................

Na Mwandishi Wetu, Mbulu DC 

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Dkt Emanuel Nuwas amekutana na watu wenye mahitaji maalumu katika jimbo hilo na kuzungumza kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kujua changamoto zao ili aweze kuzifanyika kazi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 24, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dongobesh  alisema lengo ya kikao hicho ni kuimarisha ukaribu na ushirikishwaji wa mambo mbalimbali na kundi hilo na kuona namna watakavyoweza kuinuka kiuchumi.

Wahitaji hao walioshiriki kikao hicho walikuwa na viongozi wao kutoka katika ngazi za Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji.

Baada ya kufanya kikao hicho na kusikiliza kero zao Dkt. Nuwas aliahidi kushirikiana nao kwa mambo mbalimbali ikiwemo kupata mikopo, bima kwa wote,kushirikishwa kwenye masuala ya maamuzi na upatikanaji wa vifaa saidizi kama miwani, miguu bandia ya kutembelea (Magongo),fimbo nyeupe,vifaa vya kusomea na vingine...

Aidha, Dkt Nuwas amesema hataacha kuwasemea Bungeni wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini kwa kuhakikisha Serikali inawapa kipaumbele katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa makundi yote yote.

Post a Comment

0 Comments