Misa ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Babati Mjini ambayo Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Emmanuel Khambay alihudhuria ikiendelea.
...............................
Na Mwandishi Wetu, Manyara
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay
amehitimisha sherehe ya Krismasi kwa kushiriki chakula na wahitaji.
Mhe. Khambay ametumia siku ya pili baada ya sikukuu ya krismasi
‘Boxing Day’ ambayo ni maalumu kwa kufungua zawadi kusherehekea na wahitaji kwa
kushirikiana na Vijana wa Katoliki wa Tanzania (VIWAWA) Parokia ya Roho
Mtakatifu ambapo alitoa ng’ombe kwa ajili ya kitoweo.
Sherehekea hiyo iliyofanyika Desemba 26, 2025 iliwahusisha
watoto yatima, watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambayo ilikwenda
sambamba na Misa ya shukrani
iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu .
Hafla hiyo ilifanyika Ufukwe wa Paradise uliopo Babati
Mjini.
Akizungumza katika hafla hiyo Khambay alisema ataendelea
kushirikiana na wahitaji katika masuala mbalimbali yanayowahusu na shughuli za
maendeleo kutokana na kutambua mchango walionao katika jamii licha ya kuwa na
changamoto mbalimbali.
Viongozi wa Viwawa na wahitaji wakizungumza kwa nyakati
tofauti katika hafla hiyo walimshukuru Mhe. Khambay kwa kuandaa hafla hiyo na
kuonesha jinsi anavyowajali ambapo walimuomba Mungu aendelee kumpa afya njema
na maisha marefu ya kuwatumikia wananchi wa Babati na Taifa kwa ujumla.
Hafla hiyo ilinogeshwa na burudani za nyimbo za kumtukuza
Mungu kutoka kwa Viwawa na wahitaji



0 Comments