Subscribe Us

MBUNGE JIMBO LA BABATI MJINI KESHO KUANZA ZIARA YA KIKAZI

Mbunge  wa Jimbo la Babati Mjini, Mhe. Emmanuel Khambay

............................

Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini, Mhe. Emmanuel Khambay  kesho anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi yake kesho Januari 6, 2026 atafanya ziara hiyo Kata ya Singi eneo la Gendi Barazani na Januari 2, 2026 atakuwa Kata ya  Nangara Kituo cha afya.

Januari 8 atakuwa Kata ya Sigino na atakuwa na mkutano ofisi ya Kata ya Sigino ambapo Januari 9 atakuwa Kata ya Mtuka  ambapo pia atafanya mkutano ofisi ya kata hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Januari 10, Mbunge Khambay atafanya ziara Kata ya Maisaka na kufanya mkutano ofisi ya kata hiyo ambapo Januari 11 atakuwa Kata ya Bagara eneo la Nakwa na kuhitimisha ziara hiyo Januari 12 Babati mjini eneo la Maisaka B na kutaja muda kuwa ni 8:00 Mchana.

Mhe. Khambay anawaalika wananchi wote kushiriki ziara hiyo.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale 0754362990 

Post a Comment

0 Comments