Subscribe Us

MAMA NTILIE TUNDUMA WATAKIWA KUWA WALEZI BORA KWA WATOTO WAO.

Na Issa Mwadangala.

Wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo, hasa wauza vyakula maarufu kama Mama Ntilie katika Mtaa na Kata ya Kaloleni, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe, wametakiwa kuwa walezi wa familia zao kama wanavyozingatia shughuli zao za kibiashara.

Rai hiyo imetolewa Januari 31, 2026, na Polisi Kata wa Kaloleni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sinai Mwaseba, akiwasihi wajasiriamali hao kuhakikisha wanawalea watoto wao ipasavyo ili kuweza kutambua vitendo vya kikatili vinavyoweza kutokea, hususan wakati wa shughuli za kila siku au utafutaji wa riziki zao.

Mkaguzi Sinai, alisisitiza umuhimu wa malezi bora, akiwataka wazazi na walezi kuwa makini kwa watoto wao, kuhakikisha usalama wao na kuzuia wasipate matatizo au kufanyiwa vitendo vya ukatili katika ukuaji wao.

Post a Comment

0 Comments