Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege, akizungumza na Rais Mstaafu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete leo Februari 19,.2026 alipoitembelea familia yake Kawe Jijini Dar es Salaam.
.................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
Umuhimu wa kutembea viongozi wastaafu ni Kudumisha Mshikamano na Hekima
Viongozi wastaafu ni hazina ya uzoefu na hekima iliyojengwa kwa miongo kadhaa, hivyo kutembelewa kunahakikisha busara zao zinabaki kuwa nguzo ya taifa.
Aidha, kutembelewa kwa viongozi hao kunaimarisha Umoja na Utambulisho wa Kitaifa na kuwa ziara hizo za kuwatembelea zinaonyesha mshikamano wa kisiasa na kitaifa, kuunganisha kizazi cha sasa na kilichopita.
Pia kutembelea viongozi ni kuheshimu mchango wao na ni kiashirio cha heshima kwa utumishi uliotukuka wa viongozi hao kwa taifa.
Ukaribu na Familia za Wastaafu Serikali hutumia ziara hizo kuzitembelea na kujua hali za familia za viongozi wastaafu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria na kuonyesha kujali na kuendeleza Utamaduni wa Uzalendo.
Ziara hizi zinajenga utamaduni wa kuheshimiana na kuonyesha uzalendo, zikionyesha kuwa taifa linathamini mchango wa viongozi wake.
Pia Ziara hizi husaidia kudumisha utulivu na kuendeleza misingi ya nchi, kama inavyoonekana katika juhudi za viongozi wa sasa kuendeleza uhusiano na viongozi waliotangulia.
Nimeanza kuandika makala hii kwa kuzungumzia umuhimu wa kuwajulia hali viongozi nikimkusudia Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Manyara.
Mbunge huyu kupitia nafasi yake ya Uwaziri leo Februari 19, 2026 , ameitembelea Familia ya Rais Mstaafu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwake Kawe jijini Dar es Salaam na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu alipokelewa na Mhe.Kikwete akiwa na Mkewe mama Salma.
Mhe. Regina Ndege siyo kiongozi wa kwanza kuwatembelea viongozi wastaafu, viongozi wengi wamekuwa wakifanya hivyo jambo ambalo linaleta mshikamano mkubwa wa kitaifa kwa kutambua mchango wao mkubwa kwa Taifa.
Nichukue nafasi hii kumpongeza Mhe. Regina Ndege kwa kuanza ziara ya kuwatembelea viongozi kwa kuitembelea Familia ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baade kuendelea na ziara kama hiyo kwa viongozi wengine wastaafu.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisisitiza jaambo alipokuwa akizungumza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege nyumbani kwake.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege, akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma baada ya kuzungumza nao alipowatembelea.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Regina Ndege,akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine baada ya ziara hiyo.Makala hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale, simu namba 0754362990.







0 Comments