Na Issa Mwadangala.
Wananchi wa Mtaa wa Lami Vatican, Kata ya Ilolo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe, wametakiwa kutojichukulia sheria mkononi, bali kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kushughulikia watuhumiwa wa uhalifu.
Akiongea na wananchi hao Januari 31, 2026, Polisi Kata wa Ilolo Mkaguzi wa Polisi Aggrey Mbogo, aliwashukuru kwa ushirikiano wao kwa kuwakamata watuhumiwa wa kosa la wizi katika mtaa huo, na kuwataka kuacha kujichukulia sheria mikononi mwao, huku akisisitiza kuwa hatua za kisheria ni za msingi katika kuhakikisha haki inatimizwa bila kuhatarisha amani ya jamii.
Baada ya kuwapongeza wananchi hao, Mkaguzi Mbogo aliwahimiza wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja na wageni wanaoingia katika mtaa huo bila kufuata taratibu kwani itapunguza uhalifu na kuimarisha usalama wa kila mmoja katika mtaa huo.

.png)



0 Comments