Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay akizungumza wakati wa hafla ya futari aliyowaandalia Waislamu wa Kata ya Bonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara Machi 13, 2026.
.................................
Na Dotto Mwaibale.
MAMIA ya Waislamu wa Kata ya Bonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara wameshiriki kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay Machi 13, 2026.
Halfla ya futari hiyo ilifanyika katika Msikiti wa Taqwa katika Kata ya Bonga
Mhe. Khaambay akizungumza katika hafla hiyo aliwataka waumini na wanaanchi wa kata hiyo kudumisha amani na upendo ikiwa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaania Dkt. Samia Suluhu Hassan naa viongozi mbalimbali.
Aidha, Khambay aliahidi kusimamia utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa wakati wa kampeni ya uchaguzi ikiwa ni kukamilisha mambo yote yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
" Nitasimaamia utekelezaji wa ilani ya chama chetu na kutimiza ahadi nilizoahidi kwenye kata hii," alisema Khambay.
Waumini wa Kiislamu wa kata hiyo wakiongozwa na Sheikh wao walifanya dua maalumu la kuombea taifa ambapo pia walitumia nafasi hiyo kumshukuru mbunge wao Mhe. Khambay kwa futari aliyoandaa na kumfanyia dua.
Akizungumza na wazee Mhe. Khambay aliwakabidhi fedha za kununua vifaa vya kilimo ili wajiongezee kipato.
Katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watu mbalimbali wamekuwa wakijipatia thawabu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kufuturisha wenzao walio na Swawm kama alivyofanya Mhe. Khambay pasipo kupungukiwa kitu.
Wanawake wakipata futari iliyoandaliwa na mbunge wao Mhe. Khambay.Mhe. Khambay akizungumza na wazee kwenye hafla hiyo.
Mhe. Khambay akishiriki kupata futari na wazee wa Kata ya Bonga
Wazee wakipata futari
Wanawake wakipata futari,
Shukurani zikitolewa kwaa Mbunge Khambay kwa kuandaa futari hiyo.
Shukurani zikitolewa kwa Mbunge Khambay kwa kufanya tendo jema la kiimani kwa kuandaa futari hiyo
Wazee wakiwa kwenye futari hiyo.
Shukurani zikitolewa.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.
Chanzo Nick Photo Studio.















0 Comments