Subscribe Us

UWT BABATI VIJIJINI WAUNGANA NA WANAWAKE KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Na John Walter-Babati

Wanawake wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Babati Vijijini wameungana na wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika machi 6,2026 katika viwanja vya Shule ya Msingi Vilima Vitatu, Kata ya Nkaiti.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa UWT Babati Vijijini Agatha Raphael Tsere amewakumbusha wanawake kujituma katika shughuli za maendeleo na kuacha tabia ya kuwa tegemezi.

Aidha amewahimiza wanawake kupinga kwa nguvu vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutokubali kuvifumbia macho, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa jamii kushirikiana kukomesha vitendo hivyo.

Katika sherehe hizo pia alihudhuria Katibu wa UWT Babati Vijijini Tupilike Eliya Kabejela ambaye aliungana na wanawake wengine kushiriki katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya mwaka huu yameongozwa na kaulimbiu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi wa Kufikia Dira 2050.” 

Post a Comment

0 Comments