Subscribe Us

WADAU SINGIDA WAIPONGEZA TAKUKURU VITA DHIDI YA RUSHWA

Skauti ni wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Singida, Petro Horombe akizungumza Machi 9, 2026 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026.

.................................. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

WADAU wa Mapambano dhidi ya rushwa Mkoa wa Singida wameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa hatua inazozifanya na kukabiliana na vitendo vya rushwa mkoani humo.

Wakizungumza wakati wa mkutano   na  Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Petro Horombe Machi 9, 2026 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026 waliipongeza taasisi hiyo kwa jitihada kubwa inazozifanya katika mapambano dhidiya vitendo vya rushwa.

“ Kwanza kabisa niwapongeze TAKUKURU kwa kazi kubwa walioifanya katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2025/ 2026 kwani ni mafanikio kwetu TRA,’ alisema Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Singida, Sadru Kamugisha.

Kamugisha alisema TAKUKURU imekuwa ikiwasaidia kubaini mianya ya uvujishaji wa mapato ya Serikali katika miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini kama kutotoa risiti sahihi za mapato na wao kuchukua hatua naa kufaanya mapato ya Serikali yasipotee.

Kwa upande wake Afisa Usafirishaaji wa Mkoa wa Singida, Mary Kalambo aliipongeza TAKUKURU kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo aliyahimiza makundi yote ya watu kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Mdau wa TAKUKURU kupitia Kundi la Vijana, Rashid Hamimu aalisema vitendo vya rushwa kinakatazwa na dini zote na kuwa kundi hilo linashambuliwa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira, rushwa ya ngono ambapo alihimiza kuelimishwa kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Mwanafunzi Hatba Msangi, kutoka Klabu ya mapambano ya rushwa  Shule ya Sekondari Senge, alisema klabu hiyo imekuwa ikiwasaidia kujielewa na kutambua haki zao na kuweza kuwafikia wenzao na kutoa elimu ya mapaambano dhidi ya vitendo vya rushwa.

Hatba alitumia nafasi hiyo kuipongeza TAKUKURU kwa kuanzisha klabu hizo ambazo zimewasaidia kujua madhara ya rushwa na mapambano ya kukabiliana nayo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Singida (SHIVYAWATA), Veronica Timotheo aliishukuru TAKUKURU kwa kuwapatia elimu ya uelewa wa pamoja yenye lengo la kupambana na vitendo vya rushwa.

Naye Kamishna wa Skauti Wilaya ya Ikungi Robert Michael  akimwakilisha Kamishna wa Skauti Mkoa wa  Singida,  alisema TAKUKURU ni wadau muhimu katika Chama  cha Skauti  kwenye mapambano dhidi ya rushwa na kuwa malengo makubwa ni kutoa elimu kwa vijana kupitia elimu isiyo rasmi, makambi, Semina na mafunzo mbalimbali kupitia mashuleni . 

Alisema Skauti ina klabu za kupinga rushwa katika shule za msingi, sekondari, Vyuo vya kati na Vyuo vikuu hivyo kupitia umoja huo wanasaidiana na TAKUKURU katika vita vya rushwa nchini.

Afisa Usafirishaji Mkoa wa Singida, Mary Kalambo akizungumza.
Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Singida, Sadru Kamugisha, akiipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri wanayoifanya..
Mdau wa TAKUKURU kupitia Kundi la Vijana, Rashid Hamimu, akizungumza.
Mwanafunzi Hatba Msangi, kutoka Klabu ya mapambano dhidi ya rushwa  Shule ya Sekondari Senge, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Singida (SHIVYAWATA), Veronica Timotheo akiishukuru TAKUKURU.
Kamishna wa Skauti Wilaya ya Ikungi Robert Michael, akizungumza.

 

Post a Comment

0 Comments