Subscribe Us

MKOA WA MANYARA WANG’ARA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, akiongoza uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 zilizofanyika Aprili 2, 2026 Uwanja wa Gombani, Pemba.

.....................

Na Mwandishi Wetu 

MKOA wa Manyara umeng’ara katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoani humo   Inyasi Amsi  kuteuliwa kuwa miongoni mwa wakimbiza Mwenge Kitaifa.

Hayo ni mafanikio makubwa kwa mkoa huo na kuonesha jinsi gani unavyowaandaa vijana kuwa viongozi chini ya kazi kubwa inayofanywa na mkuu wa mkoa huo Mhe. Queen Cuthbert Sendiga.

Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa umefanyika Aprili 2, 2026 Uwanja wa Gombani, Pemba  na kuongonzwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ambaye amewataka Watanzania kuendelea kulinda amani, kudumisha umoja na kuimarisha uzalendo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Mhe.Regina Ndege ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara alishiriki hafla hiyo akiwa na  Wenyeviti,  Makatibu wa UVCCM kutoka Wilaya za Mkoa wa Manyara.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Mhe.Regina Ndege akiwa na Wenyeviti, Makatibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara katika hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Pemba Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Abdi Mahamud Abdi (wa pili kushoto), akiwa na Wenyeviti. Makatibu wa umoja huo kutoka Mkoa wa Manyara wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za Mwnge wa Uhuru Pemba Zanzibar.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Manyara ambaye atakuwa ni miongoni mwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Inyasi Amsi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Grace Mali, aliyegombea Ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini kura za maoni na kushika nafasi ya tatu na  Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Manyara, CDE. John Nzwalile katika moja ya tukio la shughuli za kichama mkoani humo.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.
 

Post a Comment

0 Comments