Kwa muda mrefu nilikuwa naingia kwenye mahusiano yaliyoanza vizuri lakini yakavunjika ghafla. Kila mara ilikuwa ni hadithi ile ile mwanzo mzuri, matumaini makubwa, halafu mwisho usioeleweka. Nilijikuta nikibaki na maumivu na maswali mengi yasiyo na majibu.
Nilianza kujiuliza kama tatizo lilikuwa kwangu.
Nilijaribu kubadilika, kuwa mvumilivu zaidi, na kujitahidi kuelewa wenzi wangu. Lakini licha ya jitihada hizo zote, matokeo hayakubadilika. Ilikuwa kama mzunguko unaojirudia bila mwisho. Kadri muda ulivyopita, nilianza kupoteza imani na mahusiano kabisa.




0 Comments