Subscribe Us

𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐄𝐋𝐄𝐊𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐀𝐋𝐈 𝐑𝐖𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐍𝐘𝐔𝐊𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Kigali, Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) tarehe 19 Mei, 2026.

Mkutano huo wa Kimataifa unawakutanisha pia wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya kimataifa, ambapo utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika. Mkutano huo pia unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati.
Rais Mhe. Dkt. Samia aondoka nchini kuelekea Kigali nchini Rwanda kushiriki Mkutano wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA).

Post a Comment

0 Comments