Wajasiriamali wanaojishughulisha na uuzaji wa chakula na vinywaji wa Mjini Kondoa wakiwa kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mmlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Kati Dodoma.
.............................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Kati Dodoma imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaojishughulisha na biashara ya kuuza vyakula na vinywaji wa Wilaya ya Kondoa.
Afisa Mtafiti wa Soko la Ajira VETA Kanda ya Kati, Sadan Komungoma akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 19, 2026 alisema ni mahususi kwa wajasiriamali wanaouza chakula na vinywaji.
" Zaidi ya wajasiriamali 80 wanaojishughulisha na biashara ya kuuza chakula na vinywaji hapa mjini Kondoa wamepata mafunzo ya namna bora ya kumuhudumia mteja (Customer Care)," alisema Komungoma.
Komungoma alisema msisitizo mkubwa katika mafunzo hayo ni namna ya kuwa nadhifu wa vyombo na mavazi wakati wa kutoa huduma hizo.
Mafunzo hayo ambayo yanatolewa chini ya usimamamizi wa VETA yatafanyika kwa muda wa siku nne huku baadhi ya washiriki wakitoa pongezi kwa Serikali kwa kuweza kulikumbuka kundi hilo ambalo hutajwa kusahaulika.
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea kutolewa.







0 Comments